Breaking News

ESSAU FRANCIS (MAKUMBA) NA WENZAKE WANNE MBARONI KWA TUHUMA ZA UHALIFU

Jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es salaam linamshikilia Essau Fransis maarufu kama (Makumba) mwenye umri wa miaka 27 mkazi wa Makumbusho na wenzake wanne kwa tuhuma za kufanya na kuratibu matukio ya uhalifu jijini Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo Mei 4, 2024 kamanda SACP Muliro Muliro amesema katika Operesheni hiyo ilianza mwezi Marchi, 2024 mhutumiwa alikamatwa pamoja na wenzake nne (wanne) wakiwa na Televisheni thelathini na tano (35) zilizoibwa katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam.

"Katika operesheni kali maalum ya kuzuia, kufuwatilia wahalifu tumefanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao kwa makosa mbalimbali ikiwemo ya kuvunja nyumba na kuiba televisheni thelathini na tano (35) pamoja na vifaa mbalimbali vya kielectroniki vilizoibwa katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam." Alisema SACP Muliro.

Alisema kati ya Televisheni thelathini na tano (35) zilizokamatwa tayali Televisheni sita (6) zimeshatambuliwa  ma wamiliki wake kwa kuonyesha vielelezo mbalimbali ikiwemo risiti za manunuzi.