TCB BENKI NA METRO LIFE ASSURANCE WAJA NA ADABIMA KUTIMIZA NDOTO KIELIMU KWA WANAFUNZI PINDI WAZAZI WANAPOFARIKI
Benki ya TCB na Kampuni ya Bima "Metro Life Assurance" wa wameingia makubaliano ya kutoa huduma ya bima itakayo wawezesha watoto kuendelea na masomo baada ya wazazi ama wategemezi wao kufariki Dunia.
Akizungumza hafla ya Meneja wa TCB, Francis Kaaya amesema huduma hiyo ambayo inaitwa ADABIMA ni mahusus kwaajili ya kutimiza ndoto za watoto kuendelea na masomo pindi wategemezi wao kufariki Dunia.
"Kupitia mradi huu wa ADABIMA utatimiza ndoto za watoto za kuendelea na masomo hazitafifia mara baada ya wazazi au wategemezi watapofariki na kuwaacha wakiwa bado wanasoma,". Alisema bw. Kaaya.
Alisema mzazi ama mlezi ambaye atakuwa amewakatia bima hiyo watoto wake TCB na Metro Life Assurance watabeba jukumu la kuendelea jukumu la kuwasoma hadi watakapo hitimu masomo yao.
Aliongeza kuwa kupitia makubaliano hayo ADABIMA mzazi au mlezi atalipia asilimia sita ya ada ya mtoto wake na akiwa yuko pekee atalipia asilimia tano ya ada ya shule ya mtoto wake.
Amesema makubaliano hayo ambayo yamelemga wanafunzi wa ngazi zote kuanzia awali mpaka chuo na ikiwa mwanafunzi yupo mwaka wa kwanza Chuo chochote ataendelea kisoma hadi atakapo maliza masomo yake pamoja na kutapewa fedha ya matumizi shilingi milioni moja.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Metro Assurance, bwana Amani Boma amesema wameamua kuungana na TCB kutoa huduma hiyo kutoka na kuwa na matawi nchi nzima hali ambayo itasaidia kuwafikia wateja wengi Kwa kipindi kifupi.
"Hii ni bima inayokuja kusaidia kifedha mtoto aweze kulipa hadi atakapomaliza shule baada ya wazazi wake kufariki na ni vema wazazi wengi wakajitokeza kukata ili vijana waweze kutimiza ndoto zao ikiwa wao wataondoka Duniani, Alisema Bw. Boma.








