Breaking News

WAZIRI MKUU MAJALIWA KUFUNGUA KONGAMANO LA WAANDISHI WA HABARI WA MITANDAO YA KIJAMII MEI 20

Waziri mkuu Kasimu Majaliwa anatarajiwa kufungua kongamano lililoratibiwa na Jumuiya ya Mitandao ya Kijamii Tanzania (JUMIKITA) kwa kushirikiana na Shirikisho la Serikali za Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Tanzania TAHLISO siku ya tarehe Mei 20 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari juu ya maandalizi ya kongamano hilo la kihistoria MWENYEKITI wa jumuia hiyo bwana Shaaban Matwebe amesema Kongamano hilo litakuwa na dhima kuu ya kujadili undishi wa habari kupitia mitandao ya kijamiii pamoja na upashanaji wa habari kupitia mitandao hiyo.

"Lengo la Kongamano hilo kuwaleta pamoja waandishi wa habari kujadiliana kwa pamoja juu ya uandishi wa habari kupitia mitandao ya kijamiii pamoja na upashanaji wa habari kupitia mitandao hiyo ikiwa ni kuadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani". Alisema Bw. Matwebe.

Alisema pamoja na kuwaleta pamoja wadau wa sekta hiyo pia kongamano hilo litajadili mafanikio ya miaka mitatu ya serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na kuadhimisha miaka mitatu ya tangu kuanzishwa kwa jumuia hiyo.

Aidha, aliongeza kuwa Kongamano hilo linalotarajiwa kuwa na washiriki zaidi ya 500 Mada mbalimbali zitajadiliwa ikiwa ni pamoja na mitandao ya kijamii na uzalendo, fursa zilizopo kwenye tasnia hii, mafanikio na changamoto ili kiundeshaji wa mitandao hiyo.

Bwana Matebwe alibainisha pia kongamano hilo litatoka na mapendekeze ambayo yatakayosaidia serikali kwenye uratibu wa sera za jinsi ya kuunganisha sayansi ya uchumi wa taarifa (information economics) na uchumi wa taarifa (information economy) kwa ustawi wa nchi yetu.