MEYA KUMBILAMOTO: KUFIKA KWA DKT. NCHIMBI TAMASHA LA MTOKO WA PASAKA NI KILELEZO CHA USHIRIKIANO NA WASANII
Meya wa Jiji la Dar es Salaam mheshimiwa Omary Kumbilamoto amesema kitendo cha Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM), Balozi Emmanuel Nchimbi kufika katika tamasha la 'Mtoko wa Pasaka' ni kielelezo kuwa chama kinatambuamchango mkubwa wa wasanii wa nyimbo za Injili nchini.
Akizungumza mapema leo Aprili 20, 2025 katika.mahojiano na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili katika tamasha la "Mtoko wa Pasaka sambamba na kumuombea dua Rais Samia Suluhu Hassan.
"Kitendo cha kufika katika tamasha hili pamoja na majukumu mengi ya kitaifa ni kidhillisho tosha kuwa namna chama kilivyokuwa karibu na kutambua mchango wa wasanii hii inasaidia kuleta umoja na mshikamano katika nchi yetu". Alisema kumbilamoto.
Tamasha hilo la Mtoko wa Pasaka linalofanyika katika ukumbi wa super dome masaki jijini Dar es salaam lilawaleta pamoja wasanii wa nyimbo za Injili kutoka ndani na nje ya nchini

.png)


