CHUO CHA BAHARI DAR ES SALAAM (DMI) JIKITENI KUTOA MAFUNZO KWA VITENDO - LUDOVICK NDUHIYE
Na Mwandishi wetu - Naibu katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi Ludovick Nduhiye ametoa wito kwa uongozi wa chuo cha bahari Dar es Salaam (DMI) kuhakikisha kinajitangaza ili kiweze kujulikana ndani na nje ya nchi ili chuo hicho kiweze kupata wanafunzi wengi zaidi.
Nduhiye ameyasema hayo mara baada ya kutembelea na kukagua vifaa mbalimbali vilivyonunuliwa na Serikali kwa ajili ya kufundishia katika chuo hicho.
“Chuo hiki ni kikubwa na chuo pekee katika Afrika Mashariki na Kati hivyo ni muhimu sana kukitangaza kwani Serikali imenunua vifaa vya kisasa vya kufundishia hivyo ni muhimu sana kujitangaza ili ndani nan je kiweze kujulikana”
Kwa Upande wake Makamu mkuu wa chuo hicho Prof. Wilfred Kileo amesema kua chuo hicho kinatoa mafunzo yenye ubora wa viwango vinavyokidhi mahitaji ya kitaifa na kimataifa. Ubora huu wa viwango unatokana na usimamizi Madhubuti wa mamlaka na taasisi zilizothibitishwa na mamlaka husika husika ndani nan je nchi.
Naye Makamu Mkuu wa chuo Mipango fedha na Utawala Dkt. Lucas Mwisila amesema kuwa wa chuo hiko kinawanafunzi zaidi ya elfu tano na mwitikio ni mkubwa kwa vijana kujiunga na chuo hicho kupata mafunzo mbalimbali hasa ya ubaharia.
Vilevile Hazinaeli Machumile ni Mwanafunzi wa chuo hicho amesema kuwa kutokana na vifaa vya kisasa vya kufundishia katika chuo hicho vinawasaidia kufanya mafunzo ya vitendo kwa urahisi na kuelewa Masomo







