Breaking News

KATIBU WA JUMUIYA YA VIJANA WA CHAMA CHA CUF AJIUNGA ACT WAZALENDO

 

Dar es salaam - Aliyekuwa Katibu wa Jumuiya ya Vijana ya Chama cha Wananchi CUF (JUVICUF) na Afisa Mwandamizi katika Ofisi ya Katibu Mkuu, Idd Mkanza leo Mei 11, 2025 ametanga kujiondoa katika Chama cha CUF na kujiunga na Chama cha ACT Wazalendo.

Amesema Uamuzi wa kuachana na CUF na kujiunga na ACT Wazalendo umetokana na tafakuri ya kina niliyoifanya na kujiridhisha kuwa ni uamuzi sahihi kwa ajili ya mustakabali wangu na kwa taifa langu. 

Ametaja sababu 5 za msingi ambazo zimepelekea kufikia uamuzi huo ambazo ni chama cha CUF kupoteza msingi wake wa kuwatetea makabwela na kupigania haki sawa kwa wote. Nilijiunga CUF nikiamini ni jukwaa makini la kupigania wanyonge kwenye haki zao. Ukweli wa wazi ni kuwa CUF imeacha kutekeleza wajibu huo hivi sasa na ipo kimya kwenye mambo mengi ya msingi yanayohusu haki za wananchi.

Ametaja sababu ya pili kuwa ni kuwepo na Migogoro isiyokwisha kupelekea kukidhoofisha. CUF imekuwa kinara wa migogoro baina ya viongozi wakuu na baina ya watendaji. Hakuna jitihada zinazochukuliwa kusuluhisha migogoro hiyo na badala yake imeachwa ikidhoofishe Chama.

Sababu ya tatu ni Chama kutoendeshwa kitaasisi.Mzee wangu Prof. Haruna Lipumba ambaye ndiye Mwenyekiti wa Chama kuwa mpangaji na mwamuzi wa kila kitu, Maamuzi hayafanywi tena na vikao vya maamuzi wala mashauriano ya viongozi. Mfano wa wazi ni programu ya uchaguzi wa ndani ambayo imepangwa na Prof. Lipumba na washirika wake wa karibu bila kuhusisha vikao vya Chama.
"Huu umekuwa ndio utamaduni wa kila siku wa Prof. Lipumba kiasi kwamba Chama kimekuwa  kikiwachukia na kuwafanyia mizengwe viongozi wenye ushawishi kwenye jamii ambao wangeweza kukinusuru Chama kama vile Mh. Maftaha Nachuma, Jafari Mneke na Mbunge wa Mtwara Vijijini Shamsia Mtamba" Alisema Be. Mkanza.

Ametaja sababu ya Nne kuwa ni  kuvutia na jinsi viongozi wa ACT Wazalendo walivyo na mshikamano  (Unity of purpose) katika kutekeleza wajibu wake wa kimapambano (cause of struggle). ACT Wazalendo ndio chama kimeonesha utulivu na ukomavu katika kushughulikia changamoto za ndani na kutatua migogoro.

Aliongeza kuwa ACT Wazalendo ndio Chama cha upinzani chenye tulivu zaidi nchini hivi sasa ambacho mwanasiasa yeyote ambaye hatatanguliza maslahi yake binafsi anaweza kuvutiwa kujiunga nacho. Ninajiunga ACT Wazalendo ili kutoa mchango wangu katika ukombozi wa Taifa.
Ametaja sababu ya Tano kuwa amevutiwa na Nimevutiwa na misingi na sera za ACT Wazalendo. Nimejiridhisha kuwa hiki ni chama. kilichojikita kwenye hoja. Nimevutiwa na jinsi Chama kinavyokuza vijana kiuongozi na kuwaonesha njia. Ninaona wazi jinsi Chama kilivyojikita kwenye malengo yake na kinavyoyatekeleza na kujiimarisha. Nimevutiwa na ukweli kuwa ACT Wazalendo ni Chama kinachokua kwa kasi zaidi nchini.

Ninajiunga leo na ACT Wazalendo kwa ajili ya kuja kutoa mchango wangu katika kutekeleza malengo ya Chama kama mwanachama. Ni vizuri niseme hapa kuwa nitafanya mapambano haya nyumbani Same Mashariki, Mkoani kwangu Kilimanjaro na Tanzania kwa ujumla. Ninajiunga na ACT Wazalendo nikiwa na furaha tele kuwa nimefanya uamuzi sahihi na nimechagua jukwaa madhubuti la kisiasa.

Awali akizungumza mara baada ya kimpokea Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana taifa, ACT Wazalendo Abdul Nondo amesema moja ya ajenda ya chama ni kuongeza wanachama wapya hivyo chama kimempokea na kutoa wito kwa wale wote ambao wanaona na kuhisi awapati jukwaa la kufanya siasa au kufikia malengo nawakarisha sana.