Breaking News

MBETO AMJIBU OMO KWANINI CCM KIKO MADARAKANI KWA MUDA MREFU

Na Mwandishi  Wetu, Zanzibar - Chama Cha Mapinduzi  kimemtaka Mwenyekiti  wa ACT  Wazalendo, Othman Masoud  Othman , kutoulinganisha uimara wa CCM  na vyama vingine Barani   Afrika kwakuwa CCM ndio baba wa demokrasia  chenye Amana na  Nguvu za ushawishi  kisiasa katika jamii.

Pia  CCM kimeelezea  karibu Vyama vyote vya Siasa  Kusini mwa Jangwa la Sahara vimejifunza mbinu na mikakati ya ukombozi  ,kupigania uhuru na  Siasa  safi kutoka CCM .

Hayo yameelezwa na Katibu  wa Kamati  Maalum  ya NEC  Zanzibar ,Idara ta Itikadi , Uenezi na Mafunzo ,Khamis  Mbeto  Khamis,  aliyemtaka Othman (OMO) kuijua historia ya CCM na michango yake kwa nchi kadhaa za  Afrika .

Mbeto  alikuwa akijibu mapigo kutokana na madai ya OMO  kuwa katika  nchi kadhaa za kiafrika Vyama vya Ukombozi vimeondolewa madarakani kupitia  Uchaguzi na kukubali matokeo lakini  CCM hakitaki .

Akijibu hoja hizo,Mbeto alisema si kwamba CCM hakitaki kuondoka bali kina  nguvu  kubwa za  kisiasa ndizo zinazokifanya  hicho kiendelee kuaminiwa na wananchi na kupigiwa kura kwenye chaguzi kuu zote .

"CCM hakipo madarakani kwa kujiweka kwa shuruti .Hakiongozi kwa muda mrefu ila wananchi ndio wanaotaka kiendelee kubaki madarakani kwa sera zake  ,uaminifu na historia  yake adilifu " Alisema Mbeto 

Aidha  Katibu huyo Mwenezi alieleza kuwa Vyama vyote  vya Kisiasa havikujijenga ndani ya umma mara baada ya kupata uhuru  kama TANU/ASP na CCM vikivuoweza kujiimarisha.

"CCM kina mizizi usioweza kukatika kirahisi hata baada ya miaka hamsini toka sasa  .Kimeutumia vyema  mfumo wa chama kimoja  na kushika hatamu za utawala kisiasa,kiuchumi  na kijamii . Kuifananisha CCM na  Vyama vingine ni kukikosea  adabu "Alieleza.

Mbeto  alisema tofauti iliopo kati ya CCM na vyama vingine ikiwemo na vyama vya upinzani vya  Tanzania, CCM kimeendelea kuungwa mkono kwa sera zake za  kulinda Umoja,Amani , mshikamano na maendeleo . 

"Hakuna Seychelles, Afrika Kusini huru , Botswana, Lesotho , Angola, Msumbuji ,  Zambia ,Malawi,  Namibia bila  Tanzania  chini ya CCM  .CCM ndio mkufunzi wa siasa, maendeleo ya demokrasia na umoja wa kitaifa  "Alisiaitiza 

Mbeto  akieleza zaidi, alimtaka Othman ambaye ni Makamo wa Kwanza  wa Rais  SMZ , kutokiona CCM ni chama kidogo akakifananisha na ACT ,Chadema au CUF ambavyo vimeundwa kati ya mwaka 1993 na zaidi  ya mwaka 2000.

"Si kwamba  CCM kipo madarakani kwa muda mrefu bali kinawekwa kwa hiari ya wananchi wenyewe kwa muda mrefu .OMO atofautishe kuwekwa na kujiweka 'Aliongeza kusema.