WAZIRI WA MAMBO YA NJE Na USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI KUWASILISHA BAJETI BUNGENI
Dodoma, 28 Mei 2025 – Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Balozi Mahmoud Thabit Kombo, anatarajiwa kuwasilisha Bungeni Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara yake kwa mwaka wa fedha 2025/2026 leo tarehe 28 Mei 2025.
Uwasilishaji huo utafanyika katika ukumbi wa Bunge jijini Dodoma, ambapo Waziri Balozi Kombo atatoa muhtasari wa vipaumbele vya wizara kwa mwaka ujao wa fedha, pamoja na kueleza mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa bajeti ya mwaka uliopita.
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inashughulikia masuala ya diplomasia, ushirikiano wa kikanda na kimataifa, pamoja na kuhakikisha maslahi ya taifa yanatetewa na kuendelezwa katika ulingo wa kimataifa.




