Breaking News

TANZANIA KUANDAA MKUTANO WA 14 WA JUKWAA LA UTAWALA WA MTANDAO AFRIKA (AfIGF)

Jukwaa la Utawala wa Mtandao Barani Afrika (AfIGF) limeandaa mkutano wake mkubwa wa 14, unaotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 29 hadi 31 Mei mwaka huu. Mkutano huo utafanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Mkutano huu unawaleta pamoja wadau mbalimbali wa teknolojia ya habari na mawasiliano kutoka ndani na nje ya bara la Afrika, kujadili masuala muhimu yahusuyo usimamizi na maendeleo ya mtandao. Lengo kuu ni kuweka mikakati ya pamoja ya kuhakikisha matumizi salama, jumuishi, na endelevu ya teknolojia ya mtandao barani Afrika.

Kwa mara nyingine tena, Tanzania inaandaa jukwaa hili muhimu, ikitoa fursa kwa washiriki kubadilishana uzoefu, maarifa, na kuimarisha ushirikiano katika zama hizi za kidijitali.