Breaking News

WAZIRI MKUU MAJALIWA AMWASILISHA RAIS SAMIA KATIKA KONGAMANO LA AMANI MWANZA

Mwanza — Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, leo amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Kongamano la Amani la Afrika Mashariki lililofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Mirongo, jijini Mwanza.

Kongamano hilo limeandaliwa na The Islamic Foundation kwa kushirikiana na Safina Islamic Foundation, likiwa na lengo la kuwaleta pamoja viongozi wa dini, wataalamu, vijana, wanawake na wadau wa maendeleo kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika Mashariki.
Kwa kaulimbiu isemayo "Amani, Imani na Mshikamano", kongamano hili ni jukwaa muhimu la majadiliano kuhusu masuala ya msingi yanayoigusa jamii, ikiwa ni pamoja na kudumisha amani, kuimarisha mshikamano wa kijamii na kuendeleza maadili ya kidini na kijamii.

Waziri Mkuu Majaliwa, katika hotuba yake, alisisitiza umuhimu wa amani kama msingi wa maendeleo endelevu, huku akiwapongeza waandaaji kwa kuandaa jukwaa la kuhamasisha mshikamano miongoni mwa wananchi wa Afrika Mashariki.

Kongamano hilo limeendelea kuvutia washiriki kutoka sekta mbalimbali na linatarajiwa kutoa mapendekezo ya kisera na kijamii yatakayosaidia kuimarisha uhusiano na maelewano katika ukanda huu wa Afrika.