Breaking News

ASHA MOHAMED AJITOSA KUWANIA UDIWANI WA VITI MAALUM JIMBO LA KAWE

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kinondoni, Asha Mohamed, ameonesha nia ya kuwania nafasi ya Udiwani wa Viti Maalum kwa kuchukua fomu ya kugombea katika Jimbo la Kawe, Wilaya ya Kinondoni.

Hatua hiyo ni sehemu ya maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa, ambapo Asha ameungana na wanachama wengine wa CCM katika kutimiza haki yao ya kidemokrasia kwa kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kupitia chama hicho tawala.

Asha Mohamed ni miongoni mwa viongozi wanawake wanaotajwa kuwa na rekodi ya ushiriki wa muda mrefu ndani ya chama, huku akijipatia heshima kutokana na mchango wake katika harakati za maendeleo ndani ya Wilaya ya Kinondoni.

Uchaguzi huo unatarajiwa kuongeza ushindani mkubwa huku wagombea wakitakiwa kuzingatia taratibu na kanuni za chama katika hatua zote za mchakato wa uteuzi