Breaking News

KATIBU MKUU WA CHAUMMA AONGOZA KIKAO CHA SEKRETARIETI JIJINI DAR ES SALAM

Katibu Mkuu wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Salum Mwalim, ameongoza kikao cha Sekretarieti ya chama hicho kilichofanyika katika Ofisi ya Makao Makuu ya chama, iliyopo Kinondoni Biafra, jijini Dar es Salaam.

Kikao hicho kilijadili masuala mbalimbali ya maendeleo ya chama, ikiwa ni pamoja na kupitia maandalizi ya Mkutano Mkuu ujao wa CHAUMMA. Tarehe na eneo la kufanyika kwa mkutano huo vitatangazwa rasmi kesho kupitia mkutano na waandishi wa habari
Mkutano Mkuu huo unatarajiwa kuwa jukwaa muhimu kwa wanachama wa CHAUMMA kujadili dira ya chama na ajenda za kisiasa za siku zijazo