Breaking News

KATIBU WA DIASPORA TANZANIA, MASUD MAFTAH, AREJESHA FOMU YA UBUNGE JIMBO LA KINONDONI

Dar es Salaam, Julai 1, 2025 — Katibu wa Diaspora Tanzania, Masud Maftah, leo amerudisha rasmi fomu ya kuwania ubunge wa Jimbo la Kinondoni kupitia chama chake, ikiwa ni sehemu ya mchakato wa kuelekea uchaguzi mkuu ujao.

Maftah alikabidhi fomu hiyo katika ofisi za chama wilayani Kinondoni huku akiambatana na wafuasi na wanachama wa chama chake waliokuwa wakimshangilia. Akizungumza baada ya kurejesha fomu, Maftah alisema amejiandaa kikamilifu kuwatumikia wananchi wa Kinondoni na kusimamia maendeleo yao kwa karibu.

"Naingia kwenye kinyang’anyiro hiki nikiwa na nia ya dhati ya kuleta mabadiliko chanya, kuimarisha miundombinu, huduma za jamii na kuhakikisha sauti ya Kinondoni inasikika kitaifa," alisema Maftah.

Urejeshaji wa fomu hiyo unaashiria kuanza rasmi kwa kampeni ndani ya chama kuelekea uteuzi wa mgombea atakayewakilisha chama hicho katika uchaguzi wa ubunge utakaofanyika baadaye mwaka huu.