Breaking News

NAIBU WAZIRI MKUU AZINDUA RASMI MFUMO WA TAI-HABARI

Dar es salaam - Naibu Waziri Mkuu Mhe. Dkt. Doto Biteko akibonyesha kitufe kuzindua rasmi Mfumo wa Usajili wa Waandishi wa Habari unaojulikana kwa jina la TAI-Habari leo tarehe 09 Julai, 2025 wakati wa Mkutano wa Wadau kujadili Mchango wa Sekta ya Habari katika kufanikisha Uchaguzi Mkuu 2025 uliofanyika Ukumbi wa Mlimani City.

Kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Palamagamba Kabudi, (kushoto) Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Bw. Gerson Msigwa. Wa kwanza kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo Rodne Mbuya