Breaking News

KAIMU MKURUGENZI MKUU WA TMA ATEMBELEA BANDA LA NIT KATIKA MAONESHO YA NANENANE

Dodoma – Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dkt. Ladislaus Chang'a, ametembelea banda la Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) katika Maonesho ya Kitaifa ya Wakulima (NaneNane) yanayofanyika katika viwanja vya Nzuguni, jijini Dodoma.

Katika ziara hiyo, Dkt. Chang'a amepongeza juhudi za NIT katika kubuni na kuonyesha teknolojia zinazolenga kuongeza ufanisi na tija katika sekta ya kilimo. Ameeleza kuwa ubunifu huo ni hatua muhimu katika kuhimiza matumizi ya teknolojia katika kilimo, hatua ambayo itawezesha wakulima kuongeza uzalishaji na kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi.
Maonesho ya NaneNane mwaka huu yanafanyika kuanzia tarehe 1 hadi 8 Agosti 2025, yakibeba kaulimbiu isemayo: “Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Ufugaji na Uvuvi 2025.”

NIT ni miongoni mwa taasisi zinazoshiriki katika maonesho hayo kwa kuonyesha ubunifu na mchango wa elimu ya usafirishaji katika maendeleo ya kilimo na sekta nyingine za uzalishaji.