Breaking News

KIPANGULA: NI KOSA KUFANYA KAZI ZA KIHABARI BILA KUWA NA ITHIBATI

Dar es salaam - Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari -JAB Wakili Patrick Kipangula akiwasilisha Mada ya uzingatiaji wa Maadili na Sheria wakati wa Uchaguzi Mkuu. 

Wakili Kipangula amewasilisha mada hiyo leo tarehe 21 Agosti, 2025 kwenye Mkutano wa Wadau wa Sekta ya Habari na Utangazaji Kanda ya Mashariki kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 uliofanyika jijini Dar es Salaam,
Akifafanua kuhusu Sheria ya Huduma za Habari amesema, sura ya 229, kifungu 19 cha Sheria hiyo inatamka kuwa mtu yeyote hataruhusiwa kufanya kazi za Kihabari hadi pale atakapopewa Ithibati na Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari.

Wakili Kipangula amesema waandishi wanapaswa kuzingatia Sheria, Kanuni na Miongozo inayohusu Uandishi wa Habari na Utangazaji wa Habari za Uchaguzi, huku akizitaja Sheria ya Huduma za Habari na Sheria ya Uchaguzi kuwa zinahusika zaidi.
Mkutano huo umeandaliwa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) pamoja na Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari