NCAA YATUNUKIWA CHETI CHA UDHAMINI KIKAO CHA WENYEVITI WA BODI NA WAKUU WA TAASISI
Arusha - Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Dotto Biteko, amemkabidhi cheti Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Jenerali Mstaafu Venance Mabeyo, kwa kutambua mchango wa NCAA kama mmoja wa wadhamini wa kikao cha Wenyeviti wa Bodi na Wakuu wa Taasisi kilichofanyika jijini Arusha kuanzia tarehe 23 hadi 26 Agosti 2025.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Dkt. Biteko aliipongeza NCAA kwa kujitolea kushirikiana na taasisi nyingine katika kuunga mkono maendeleo ya kitaifa kupitia ushirikiano wa wadau mbalimbali.
Aidha, Mwenyekiti wa Bodi, Jenerali Mstaafu Mabeyo, alipokea cheti hicho kwa niaba ya NCAA na kueleza dhamira ya taasisi hiyo kuendelea kushirikiana na wadau wote katika kulinda urithi wa Taifa na kusaidia juhudi za maendeleo.
Hafla hiyo ilihudhuriwa pia na Kamishna wa Uhifadhi wa NCAA, Bw. Abdul-Razaq Badru, pamoja na viongozi wengine wa Serikali na taasisi mbalimbali.