RAIS SAMIA ATUMIA TRILIONI 1.3 KUBORESHA ELIMU BILA ADA
Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imewekeza shilingi trilioni 1.3 katika mpango wa elimu bila ada kuanzia elimu ya awali hadi kidato cha sita. Hatua hii imechangia kuimarika kwa miundombinu ya elimu na kuongeza idadi ya wanafunzi nchini.
Takwimu zinaonyesha kuwa vyumba vya madarasa ya elimu ya msingi vimeongezeka kutoka 128,425 mwaka 2020 hadi 155,330 mwaka 2024, huku vya sekondari vikiongezeka kutoka 46,928 hadi 81,052 katika kipindi hicho.
Kuimarika kwa miundombinu hiyo kumepelekea ongezeko la wanafunzi kutoka 14,940,925 mwaka 2020 hadi 16,155,281 mwaka 2024.
Serikali pia imeongeza bajeti ya elimu bila ada kutoka shilingi bilioni 312 mwaka 2020 hadi trilioni 1.3 mwaka 2024, hatua iliyowezesha wanafunzi wengi zaidi kupata elimu bora na kwa usawa nchini.