Breaking News

CHINI YA RAIS SAMIA: TRILIONI 1.3 ZAWEKEZWA MIRADI YA MAJI SAFI, WANANCHI MILIONI 6 WAFAIDIKA

Serikali imetumia shilingi trilioni 1.3 kutekeleza Mradi wa Maji katika miji 28 nchini, chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan. Kupitia mradi huo, wananchi 5,985,500 wamenufaika kwa kupata huduma ya maji safi na salama.

Mradi huo umeimarisha upatikanaji wa maji katika miji mikubwa na midogo, hatua inayosaidia kupunguza milipuko ya magonjwa yatokanayo na maji machafu. Aidha, huduma hiyo imeongeza ufanisi wa wananchi katika sekta za kilimo, viwanda, elimu na afya kwa kuwawezesha kutumia maji kwa shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi.

Serikali imesisitiza kuwa itaendelea kuboresha miradi ya maji nchini ili kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma ya uhakika na endelevu.