CHINI YA UONGOZI WA RAIS SAMIA, UJENZI NA UKARABATI WA MELI YA KISASA YA MT SANGARA WAKAMILIKA
Muonekano wa meli ya mafuta ya Mv Sangara inayofanya safari zake katika Ziwa Tanganyika kwenda nchini Burundi na DR Congo.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, imekamilisha ukarabati wa meli ya mafuta ya MT Sangara inayotoa huduma katika Ziwa Tanganyika.
Meli hiyo yenye uwezo wa kubeba lita 400,000 za mafuta inatarajiwa kuchochea biashara ya majini kati ya Tanzania, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Burundi na Zambia, hatua itakayochangia kuimarisha uchumi wa mikoa ya magharibi mwa Tanzania.
Mradi huo wa ukarabati umegharimu takribani dola milioni 3 (sawa na shilingi bilioni 7.8), na ni sehemu ya juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita katika kuboresha miundombinu ya usafiri wa majini nchini.





