DKT. SAMIA AENDELEA NA KAMPENI MKOANI MTWARA, AAHIDI KUIMARISHA KILIMO, MIUNDOMBINU NA HUDUMA ZA JAMII
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameendelea na kampeni zake mkoani Mtwara, akihutubia wananchi katika maeneo ya Mangaka (Nanyumbu), Masasi na Nakapanya. Katika mikutano hiyo, Dkt. Samia ameeleza mafanikio yaliyopatikana katika kipindi chake cha uongozi na kuahidi kuendeleza jitihada za kuimarisha maisha ya Watanzania kupitia sekta za kilimo, miundombinu, huduma za jamii na biashara.
Akiwa Mangaka – Nanyumbu
Dkt. Samia amesisitiza dhamira ya serikali kuendeleza kilimo bora kwa wakulima kupitia ruzuku za pembejeo na mbolea, hatua iliyowezesha ongezeko kubwa la uzalishaji wa mazao ya biashara na chakula. Amesema uzalishaji wa korosho umeongezeka kutoka tani 15,000 hadi 24,000, na kuwaingizia wakulima zaidi ya shilingi bilioni 73. Aidha, mazao mengine kama karanga, ufuta na mbaazi yameongezeka kwa kiwango kikubwa, na kuwaongezea kipato wakulima wa mkoa huo.
Vilevile, amesema miradi ya visima vya umwagiliaji katika maeneo ya Likokona, Lukula na Masugulu ipo hatua za mwisho kukamilika, ili kuongeza tija katika kilimo cha umwagiliaji.
Katika miundombinu, Dkt. Samia ameahidi kukamilisha mradi mkubwa wa gridi ya umeme wenye thamani ya shilingi bilioni 307 kutoka Songea–Tunduru hadi Masasi, ukiwa na vituo vya kupooza umeme Tunduru na Masasi, ambapo ujenzi wa kituo cha Tunduru umeshafikia asilimia 50.

Aidha, ameahidi kuboresha barabara za lami mjini Mangaka na barabara za kuunganisha wilaya na mikoa, sambamba na kujenga madaraja. Kuhusu wafugaji, serikali imepanga kuongeza maeneo ya malisho kutoka ekari milioni 3.4 za sasa hadi kufikia milioni 6 ifikapo mwaka 2030.
Akiwa Masasi
Katika mkutano wake Masasi, Dkt. Samia ameahidi kuendeleza ruzuku za pembejeo, mbolea na viuatilifu kwa wakulima, pamoja na chanjo za mifugo kwa wafugaji. Amesema serikali itaendelea kujenga skimu za umwagiliaji ili kuongeza uzalishaji mara mbili kwa mwaka, na kongani za viwanda katika kila wilaya ili kuongeza thamani ya mazao.
Kuhusu umeme, ameeleza kuwa mradi wa kusafirisha umeme kutoka Ruvuma–Tunduru hadi Masasi unaendelea kutekelezwa, huku katika sekta ya barabara akiahidi kukamilisha barabara ya Mnivata–Newala–Masasi na sehemu ya barabara ya Minivata–Mtesa yenye urefu wa kilomita 100 kwa kiwango cha lami.
Kwa huduma za jamii, Dkt. Samia amesisitiza kuwa serikali itaendelea kuhakikisha upatikanaji wa maji safi, kukamilisha vituo vya afya na kuendeleza miundombinu ya elimu. Ameeleza pia kuwa serikali inapanga kuunganisha bandari ya Mtwara na Bambabay kupitia reli, ili kuongeza fursa za biashara na usafirishaji. Aidha, amewahakikishia wafanyabiashara wadogo, wakiwemo bodaboda, bajaji na wamachinga, kwamba serikali itabaki karibu nao kwa kuwapatia masoko na mitaji kupitia halmashauri.
Akiwa Nakapanya
Akiwa Nakapanya, Dkt. Samia ameahidi kukamilisha ujenzi wa kituo cha afya cha Namiungo pamoja na vituo na zahanati ambavyo havijakamilika. Ameeleza kuwa serikali itaendelea kusimamia upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi wote, huku hatua inayofuata katika sekta ya nishati ikiwa ni kuunganisha vitongoji vyote kwenye umeme.
Katika sekta ya kilimo, ameeleza kuwa ruzuku za pembejeo zitaendelezwa na skimu mpya za umwagiliaji na mabwawa kujengwa ili wakulima wazalishe mara mbili kwa mwaka. Pia, amesema serikali imenunua ndege zisizo na rubani (drones) tano kwa ajili ya kudhibiti wanyama waharibifu katika maeneo yenye changamoto kubwa.
Kuhusu bei za mazao, Dkt. Samia ameeleza kuwa serikali ipo kwenye mazungumzo na masoko makubwa ya kimataifa, ikiwemo India, kuhakikisha bei za mazao hazianguki zaidi ya asilimia 60 ya bei ya dunia, ili kulinda kipato cha wakulima.