Breaking News

ETDCO YAJITANGAZA MAONESHO YA KIMATAIFA EXPO 2025, JAPAN.

Osaka, Japan - Katika kuadhimisha Wiki ya Nishati katika Maonesho ya Dunia Expo 2025, Osaka, Japan, Kampuni ya ETDCO imeendelea kujitangaza kimataifa, huku wageni kutoka mataifa mbalimbali wakipata fursa ya kujifunza na kuelewa zaidi kuhusu mchango wa kampuni hiyo katika sekta ya ujenzi wa miundombinu ya umeme nchini Tanzania.

Wageni wamepata fursa ya kufahamu kazi zinazotekelezwa na ETDCO, ikiwemo miradi ya kimkakati inayolenga kuimarisha upatikanaji wa umeme nchini Tanzania, pamoja na mipango ya kukuza ushirikiano na teknolojia mpya kutoka mataifa mbalimbali duniani.
Washiriki wa maonesho hayo wameendelea kuonesha hamasa ya kujua zaidi kuhusu nafasi ya Tanzania katika sekta ya nishati, huku ETDCO ikitumia jukwaa hili kujenga mahusiano mapya, kubadilishana uzoefu pamoja na kutangaza fursa za uwekezaji.

Ushiriki wa ETDCO katika maonesho haya makubwa ni hatua muhimu ya kuimarisha taswira ya Kampuni kimataifa na kuonyesha dhamira yake ya kuchangia maendeleo ya nishati endelevu duniani.