Breaking News

HUDUMA ZA AFYA YA MAMA NA MTOTO ZABORESHWA CHINI YA RAIS SAMIA

Huduma za afya ya mama na mtoto zimeendelea kuimarika nchini chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, kufuatia kuanzishwa kwa vitengo maalum vya Neonatal Care Unit na Kangaroo Mother Care katika hospitali zaidi ya 150, vikiwemo vituo vipya 114.

Hatua hiyo imechangia ongezeko kubwa la akina mama wanaojifungulia katika vituo vya afya, kutoka asilimia 64 mwaka 2020 hadi asilimia 84 mwaka 2025.
Aidha, vifo vya watoto wachanga vimepungua kutoka 27 kwa kila vizazi hai 1,000 mwaka 2020 hadi 20 kwa kila vizazi hai 1,000 mwaka 2025, hatua inayotajwa kuwa mafanikio makubwa katika kupunguza vifo vya watoto wachanga nchini.