Breaking News

NAIBU WAZIRI CHUMI ATETA NA VIONGOZI WA AFRIKA KANDO y6a MKUTANO WA TABIANCHI ADDIS ABABA

Addis Ababa, Ethiopia - Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Cosato Chumi, ameshiriki katika Mkutano wa Pili wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Afrika kuhusu Tabianchi unaofanyika jijini Addis Ababa, Ethiopia.

Kando ya mkutano huo, Mhe. Chumi alipata fursa ya kusalimiana na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Mhe. Mahmoud Ali Youssouf, pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Angola, Mhe. Tete Antonio.
Mkutano huo unalenga kujadili hatua za pamoja za Bara la Afrika katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi na kusisitiza mshikamano wa nchi wanachama katika utekelezaji wa mikakati ya kulinda mazingira na kukuza maendeleo endelevu.