NGORONGORO YABUNI SULUHU ZA CHANGAMOTO ZA MAJI VIJIJINI
Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), kupitia Idara yake ya Maendeleo ya Jamii, imeendelea kushirikiana na vijiji vilivyopo ndani na nje ya hifadhi katika kutatua changamoto za upatikanaji wa maji, hasa kipindi hiki cha kiangazi.
Katika ziara za uhamasishaji zilizofanyika hivi karibuni katika vijiji vya Alchaniomelok, Ngoile, Meshili na Oroirobi, wakazi walipata nafasi ya kushirikiana na Mamlaka hiyo kutafuta suluhu endelevu za tatizo la maji.
NCAA imerejea tena dhamira yake ya kuboresha huduma za maji katika maeneo hayo, ikilenga kupunguza changamoto za muda mrefu zinazowakabili wananchi.
Hatua hii ya tathmini na ufuatiliaji inalenga kuhakikisha miundombinu ya maji inaendelea kufanya kazi kwa ufanisi, ili kuwawezesha wananchi kuendesha shughuli zao za kila siku na za kiuchumi kwa uhakika na ustahimilivu zaidi.








