MABALOZI WA UMOJA WA ULAYA WAKUTANA NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE KUJADILI MASUALA YA KISIASA NA UTAWALA BORA
Dar es salaam - Balozi wa Umoja wa Ulaya pamoja na Mabalozi wa nchi wanachama wa Umoja huo wamekutana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Mahmoud Thabit Kombo kwa mazungumzo ya wazi na yenye tija kuhusu maendeleo ya kisiasa nchini Tanzania.
Katika mazungumzo hayo, pande hizo mbili zimejadili masuala mbalimbali ikiwemo maandalizi ya uchaguzi ujao, kuimarisha misingi ya demokrasia, na kukuza utawala bora.
Mazungumzo hayo yameelezwa kuwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya katika kuendeleza demokrasia, utawala wa sheria na maendeleo endelevu nchini.










