Breaking News

MAHAKAMA YA KIJESHI DRC YAMHUKUMU KIFO RAIS MSTAAFU JOSEPH KABILA KWA USALITU NA UHALIFU MKUBWA

Jumanne, tarehe 30 Septemba 2025, mahakama imetoa hukumu nzito dhidi ya rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Joseph Kabila Kabange, anayejulikana pia kwa jina la Hyppolite Kanambe.

Kwa mujibu wa hukumu hiyo, Kabila amehukumiwa kifo baada ya kupatikana na hatia ya kujipatia madaraka kwa njia ya udanganyifu, kwa madai kwamba aliacha uraia wake wa Rwanda ili kuingia madarakani kinyume cha Katiba ya DRC.

Zaidi ya adhabu ya kifo, mahakama imeamuru Kabila kulipa dola bilioni 30 za Kimarekani (sawasawa na thamani yake kwa francs congolais) kwa Serikali ya DRC, pamoja na kunyang’anywa mali zake zote.

Aidha, Kabila anatakiwa kulipa fidia ya dola bilioni 2 kwa kila moja ya taasisi mbili:
 • Jimbo la Kivu Kaskazini, na
 • Mji wa Isiro,

kama sehemu ya malipo ya uharibifu.

Kwa kuwa Kabila bado ni seneta wa maisha, atakabiliwa pia na mashtaka zaidi ya 120 mbele ya mahakama ya kijeshi, yakiwemo yale ya uhalifu mkubwa na ubadhirifu wa mali ya umma.