Breaking News

𝗠𝗪𝗘𝗡𝗘𝗭𝗜 𝗞𝗘𝗡𝗔𝗡𝗜 𝗔𝗠𝗧𝗔𝗞𝗔 𝗛𝗘𝗖𝗛𝗘 𝗞𝗨𝗧𝗢𝗘𝗡𝗗𝗘𝗞𝗘𝗭𝗔 𝗦𝗜𝗔𝗦𝗔 𝗞𝗔𝗧𝗜𝗞𝗔 𝗠𝗔𝗜𝗦𝗛𝗔 𝗡𝗔 𝗠𝗔𝗧𝗔𝗧𝗜𝗭𝗢 𝗬𝗔 𝗪𝗔𝗧𝗨

𝘼𝙢𝙩𝙖𝙠𝙖 𝙠𝙪𝙟𝙞𝙚𝙡𝙚𝙢𝙞𝙨𝙝𝙖 𝙣𝙖 𝙠𝙪𝙛𝙖𝙝𝙖𝙢𝙪 𝙢𝙖𝙨𝙪𝙖𝙡𝙖 𝙢𝙗𝙖𝙡𝙞𝙢𝙗𝙖𝙡𝙞 𝙠𝙖𝙗𝙡𝙖 𝙮𝙖 𝙠𝙪𝙟𝙞𝙩𝙤𝙠𝙚𝙯𝙖 𝙠𝙪𝙯𝙪𝙣𝙜𝙪𝙢𝙯𝙖 𝙣𝙖 𝙫𝙮𝙤𝙢𝙗𝙤 𝙫𝙮𝙖 𝙝𝙖𝙗𝙖𝙧𝙞.

Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu. 𝗞𝗲𝗻𝗮𝗻𝗶 𝗞𝗶𝗵𝗼𝗻𝗴𝗼𝘀𝗶 ameeleza kuwa Dunia nzima imeathirika na kupanda kwa bei ya mafuta na kusisitiza kutoendekeza siasa katika maisha na matatizo ya watu huku akimtaka Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bw. John Heche, kujielimisha na kufahamu vyema masuala mbalimbali kabla ya kujitokeza na kuzungumza na Vyombo vya habari.

Ameeleza hayo wakati akiunguruma na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari leo Aprili 07, 2026 katika ukumbi wa White House ulipo Makao Makuu ya CCM Jijini Dodoma.

Hatua hiyo imekuja ikiwa ni siku moja mara baada ya Heche kuzungumza na Wanahabari na kuikosoa serikali kwa kushindwa kusimamia sekta ya mafuta na mfumuko wa bei uliopo na uliotokana na vita vinavyoendelea katika ukanda wa Mashariki ya Kati, ambapo pia akimshauri Heche kumuachia Afisa habari wao wa CHADEMA kufanya kazi hiyo.

"Duniani kote hakuna serikali au Chama cha siasa kinachofurahia changamoto za wananchi. Changamoto hii ya mafuta ni ya dunia nzima, nchi mbalimbali mpaka zenye uwezo mkubwa zinapita katika changamoto hii."

"Wajibu wetu wa kwanza ni tuwe wa kweli na inapotokea changamoto tusibebe siasa katika maisha ya watu. Jana kuna kiongozi amezungumza baadhi ya mambo ambayo pia hana uelewa nayo sasa Mimi nimtake ajielimishe zaidi, aujue uchumi, usiongee kitu kama hukifahamu, tafuta muda, soma, jifunze na ukishakuwa na uelewa ndio ujitokeze uongee."

Katika kuyapa nafasi maoni ya Watanzania ikiwa ndio utaratibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mwenezi Kenani, amezungumzia kuhusu maoni ya watu waliopendekeza serikali kufuta kodi kwenye mafuta na kusisitiza kuwa serikali inaendelea kutafuta suluhu ya kudumu ya udhibiti wa kupanda kwa gharama ya mafuta nchini.