Breaking News

KATAMBI: SITAKUBALI TAIFA LIANGAMIE KWA MASLAHI BINAFSI YA WACHACHE

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, amesema hataki kuona taifa likiangamia kutokana na maslahi binafsi ya baadhi ya watu wanaokiuka haki za wananchi wengi.

Katambi ametoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na wazee pamoja na wanachama wa Baraza la Ushauri la Manispaa ya Shinyanga, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Kupinga Ukatili kwa Wazee Duniani yaliyofanyika mkoani Shinyanga.

Katika hotuba yake, amesisitiza kuwa hakuvunja sheria kwa kupiga marufuku mikutano ya kisiasa, akieleza kuwa hatua hiyo ililenga kulinda usalama, amani na maslahi mapana ya taifa.