Breaking News

SERIKALI HAINA MZAHA KULINDA WATANZANIA

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema Serikali haina mzaha katika kulinda Watanzania na rasilimali za nchi, akisisitiza kuwa masuala ya usalama hayana upendeleo wala upande.

Akizungumza na wananchi wa Ikungi mkoani Singida leo Juni 27, 2026, Dkt. Mwigulu amesema Serikali imejifunza kutokana na matukio yaliyotokea mwishoni mwa mwaka 2025 yaliyowaumiza Watanzania, akisema haitaki kuona yanajirudia tena.

Ameeleza kuwa usalama wa nchi ni wa wote na hauna makundi, akibainisha kuwa licha ya kuwepo kwa vyama vya siasa, msingi mkubwa ni kulinda taifa kwanza kabla ya tofauti za kisiasa.

Aidha, amesema Serikali imebaini kuwepo kwa watu wasioitakia mema Tanzania wanaojaribu kuwatumia vijana kwa maslahi yao binafsi, na kusisitiza kuwa hatua madhubuti zinaendelea kuchukuliwa kuhakikisha nchi inabaki salama.