Breaking News

DC KISARAWE ASISITIZA WAZAZI KUWAPELEKA WATOTO KUPATA CHANJO YA POLIO YA MATONE

KISARAWE - Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mhe,Petro Magoti, leo Agosti 27, 2026, amezindua rasmi zoezi la utoaji wa chanjo ya polio ya matone kwa watoto chini ya umri wa miaka 10 katika Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe
Zoezi hilo linawalenga watoto 43,491 katika vijiji 65 vya wilaya ya Kisarawe, ambapo chanjo itatolewa katika vituo 46 kuanzia Agosti 27 hadi 30, 2026, bila malipo

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkuu wa Wilaya amewataka wazazi na walezi kuhakikisha watoto wao wanapata chanjo hiyo
“Nitoe Wito Kwa vyombo vya habari kutumia majukwaa yao kuhakikisha taarifa hizi za Chanjo zinawafikia wananchi ili kuhakikisha watoto wote wanaolengwa wanapata chanjo hiyo.” alisema DC Magoti Kisarawe

Zoezi la utoaji wa chanjo ya polio ni juhudi za serikali kuongeza ulinzi wa mtoto na jamii Kwa ujumla, hivyo wazazi na walezi wanatakiwa kuwapeleka watoto wao katika vituo vilivyotengwa.