WIZARA YA HABARI NA WADAU WAKUTANA KUJADILI NAMNA YA KUBORESHA SERA YA SANAA ZA MAONESHO
Kaimu
Mkurugenzi Maendeleo ya Sanaa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Bi. Leah Kihimbi (kushoto) akizungumza na wadau wa Shirikisho la
Sanaa za Maonesho kuhusu mikakati ya kuboresha sekta ya sanaa za
Maonesho leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkurugenzi Msaidizi Lugha
Bibi. Shani Kitogo na kulia ni Afisa Uchumi kutoka Wizara hiyo Bw.
Richard Kundi.Na Anitha Jonas – WHUSM
Rais
wa Shirikisho la Sanaa za Maonesho Bw. William Chitanda akieleza
changamoto za shirikisho kwa watendaji wa Wizara ya Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo (hawapo pichani) wakati wa kikao cha kuweka mikakati ya
kuboresha sekta ya sanaa za Maonesho leo jijini Dar es Salaam.
Katikati ni Bw. Efraim Zakaria kutoka kikundi cha Watoto Arts
Organization (WAAO).
Katibu
wa Kikundi cha Binti Leo Bi. Agness Lukanga (katikati) akieleza
utendaji wa kikundi chao kwa watendaji wa masuala ya Sanaa na
Utamaduni wakati wa kikao cha kuweka mikakati ya kuboresha sekta ya
sanaa za Maonesho leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mjumbe wa Chama
cha Sanaa za Maonesho Tanzania Bw. Nkwama Ballanga.
Mjumbe
wa Kikundi cha Sherehe Arts Association (SAA) Bi. Columba Samjela
akiwaeleza watendaji wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
(hawapo pichani) mikakati waliyonayo ya kuimarisha Sanaa leo jijini
Dar es Salaam. Kushoto ni Mjumbe wa (SAA) Bi. Grace Meena.
Mjumbe
wa Shirikisho la Sanaa za Maonesho Bw. Denis Mango akifafanua shughuli
za shirikisho katika kikao kilichofanyika Juni 21,2016 Jijini Dar es
Salaam na Watendaji wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Katikati ni Bw. Omari Kichapwi, Mjumbe wa Umoja wa Washairi Tanzania
(UWASHATA).
Mjumbe
wa Kikundi cha Umoja wa Washairi Tanzania (UWASHATA) akieleza jambo
kwa Watendaji wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo (hawapo
pichani) kuhusu umuhimu wa Sanaa ya Mashairi. Kulia ni Mjumbe wa
UWASHATA Bi. Sikuzani Jalala.
Baadhi
ya wadau wa Sanaa za Maonesho walioshiriki kikao na watendaji wa Wizara
ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakimsikiliza kwa makini
Mkurugenzi Msaidizi Lugha kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Bibi. Shani Kitogo (hayupo pichani) alipokuwa akifafanua jambo
kuhusu fani ya ushariri leo jijini Dar es Salaam.
Mjumbe
wa Chama cha Sanaa za Maonesho Tanzania Bw. Nkwama Ballanga akitoa
maoni ya kuboresha sekta ya Sanaa za Maonesho kwa watendaji wa Wizara
ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo (hawapo pichani) leo jijini Dar
es Salaam. Wapili kushoto ni Mjumbe wa UWASHATA Bi. Sikuzani Jalala.



