Kauli Ya Meya Wa Jiji Mhe. Isaya Mwita Kufatia Uvumi Ni Mmoja Wa Wanaotaka Kutimkia Ccm..

TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI KUTOKA KWA MSTAHIKI MEYA WA JIJI LA DAR ES SALAAM ISAYA
MWITA KUHUSU KANUSHO LA KUDAIWA KUTAKA KUHAMA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO
CHADEMA.
Ndugu waandishi wa habari:
Nimeshikwa na mshtuko, simanzi baada ya kusambaa kwa taarifa ambazo naweza
kusema kuwa ni za uzushi kwamba ninampango wa kujiondoa ndani ya Chama Cha
Demokrasia na Maendeleo Chadema. naomba taarifa hizo zipuuzwe mana hazina ukweli
wowote na kwamba zinampango wa kunichafua mimi pamoja na Chama Changu.
Ndugu waandishi wa habari :
Napenda ieleweke kuwa sijawahi kudhani wala kufikiria kuhama Chadema na kwenda
kwenye chama chochote kile cha siasa. Chadema ni chama ambacho nimetoka nacho
mbali tangu mwaka 2004 hadi leo, nimejenga chama kwa gaharama zangu mwenyewe.
Ndugu waandishi wa habari: Leo
nimekuwa Meya wa jiji la Dar es Salaam kupitia Chama Changu cha
Chadema,natambua kuwa chama kimeniheshimu sana kwa kunipa nafasi hii hivyo sina
sababu ya kuondoka kwani ninania ya kuwatumikia Wananchi ambao wameniamini na
wamenichagua kwa mapenzi yao wakiamini kuwa nitawaletea Maendeleo nikiwa ndani
ya Chama Cha Chadema.
Nafahamu tuhumahizi zinatokana
na aina ya utendaji wangu katika Jiji la Dar es Salaam kwani nimekuwa nikifanya
kazi badala ya kupambana na serikali pale ambapo watu wanaamini kuwa mambo
hayajaenda sawa.
Ndugu waandishi wa habari: Kukaa
kwangu kimya huku ,kutokufanya siasa za kiharakati ndani ya jiji la Dar es
Salaam haimanishi kwamba nipo upande wowote ama kukihujumu chama changu. Ila
huu ni mfumo ambao nimeuchagua na kujijengea kwa ajili ya kuwatumikia wananchi
nasio kufanya harakati za kisiasa kwakuwa nina nia ya kufanya maendeleo ndani
ya jiji la Dar es Salaam.
Ndugu waandishi wahabari: Naomba
ifahamike kuwa hakuna Mkurya ambaye aliwahi kuwa msaliti,katika nafasi yoyote
ambayo aliwahi kuwa nayo. Kutokana na historia hiyo, naomba niaminike na
wanachama na wananchi wote kuwa haitakuja kutokea Mkurya mimi nikakisaliti
chama changu.
Nakama itakuja kutokea nikafanya
hivyo ninaweza kuhatarisha maisha yangu, Familia yangu, na hivyo kujikuta
nikaingia kwenye matatizo makubwa ambayo kimsingi sio mazuri. Mama yangu ni
mjane, kama itafanya hivyo Chadema wote Mkoa wa Mara hawawezi kuwaacha ndugu
zangu salama .
Ndugu waandishi wa habari : Tangu
nimeona watu wote waliohama ,kusaliti vyama vyao, maisha yao yamekuwa mabaya,
nahata imani kwa Wananchi wao imepungua. Hivyo na Mimi sitaki kuwa kama wao,
ninania ya dhati ya kukitumikia chama changu kwa uaminifu mkubwa kama ambavyo
wao wameniamini.
Kuliko kuhama Chadema ni heri
mkanitafutie Mahala pengine pakuishi ambapo itakuwa ni mbinguni lakini sio hapa
duniani ama kwenda kwenye Chama kingine chochote cha kisisasa. Kikubwa napenda
kuwaeleza wana chama wote wa Chadema kuwa hivi sasa kila mmoja tujielekeze kwa
nguvu zetu zote kwenye kampeni hivi za uchaguzi mdogo wa madiwani unaotarajiwa
kufanyika Novemba 26 mwaka huu.msikubali kutolewa kwenye maandalizi ya
uchaguzi.
Imetolewa leo Novemba 23/2017
Christina Mwagala, Ofisa Habari
na Msemaji Mkuu wa Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam.



