DC MAKORI: VITENDO VYA UKATILI WA KIJINSIA BADO CHANGAMOTO KUBWA KATIKA JAMII
Mkuu Wa Wilaya Ya Ubungo Mhe.Kisari Makori Akiongongea Katika
Mkutano Huo.
Na Sala Mlawas:
Wito umetolewa kwa maafisa ustawi wa jamii wa kata na wilaya
kushirikiana na jeshi la polisi kupinga ukatili wa jinsia kwa wakina mama na
watoto.
Akizungumza jijini dar es salaam Mkuu
wa Wilaya ya Ubungo mhe.kisari makori alisema takribani zinaonyesha kuwa wanawake
4 kati ya 10 wamewahi kukutana ukatili wa kijinsia tangu wakiwa na miaka 15 .
Alisema tafiti zinaonyesha kuwa asilimia
42 wanawake walioolewa wanapata shida kubwa sana dhidi ya ukatili wa kijinsia
unaofanywa na wanaume zao.
Mhe..makori alisema serikali ya awamu
ya tano imejipanga vizuri kuhakikisha inatekeleza kuandaa mipango sera na mikakati
katika kuhakikisha watokomeza manyanyaso kwa mwanamke sambamba na vitendo vya
ukatili wa kijinsia unaofanywa na watu wengi katika jamii.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Wa TGNP Bi Grace Kisetu Akifafanua
Jambo Katika Mkutano Huo.
Kwa upande wake kaimu mkurugenzi mtendaji wa TGNP Bi Grace
kisetu alisema tayali wameshafanya utafiti katika shule zilizopo katika
halimashauri ya ilala, kinondoni na Ubungo kujua matatizo ya wanafunzi
yanayopelekea ukatili wa kijinsia unavyotokea mashuleni.
Alisema kupitia utafiti waliofanya
wamegundua changamoto zinazowakabili watoto wa kike ambazo zinapekekea kuwepo
na matukio ya ukatili wa kijinsia ni miundombinu mibovu ya shule hususani
ukosefu wa maji, ukosefu wa mataulo ya dharura yakujisitiri pindi wanapotokewa
na hedhi wakiwa shuleni ili waweze kujisitiri na kuendelea na masomo yao .
Aidha Bi kisetu ametoa wito kwa wanafunzi hao kushirikiana nao bega kwa bega katika vilabu vya kutoka elimu ya jinsia kwani lengo lao kubwa ni kupinga ukatili wa jinsia .
Mmoja Wa Wanafunzi Walioshiriki Katika Vilabu Vya Ukatili Wa
Kijinsia Akiongea Kwa Niaba Ya Wenzake.
Nae
mmoja wa wanafunzi walioshiriki katika vilabu vya ukatili wa kijinsia ameomba serikali
za mitaa zitenge bajeti kwa manunuzi ya taulo za kijistiri (PEDI) mashuleni
ziwasaidie watoto wakike pindi wanapopata hedhi ya dharura pamoja na kuwatengea
chumba chao kwa ajili ya kujisitiri .
Washiriki wa mkutano huo wakimsikiliza mgeni rasmi (hayupo
pichani)








