Mkutano Wa Nchi Za Kiislamu Watambua Jerusalem Ya Mashariki Kama Mji Mkuu Wa Palestina
Mkutano wa nchi za kiislamu uliofanyika jana mjini Istanbul
umetangaza kuitambua Jerusalem Mashariki kuwa mji mkuu wa Palestina, ukijibu
uamuzi wa Marekani ulioipendelea Israel.
Rasimu ya taarifa ya pamoja
iliyotolewa na jumuiya ya nchi za kiislamu OIC, imezitaka nchi zote duniani
kuitambua Palestina na sehemu ya Jerusalem Mashariki inayokaliwa kuwa mji wake
mkuu.

Wakuu
wa nchi waliohudhuria mkutano huo, wamesema uamuzi wa upande mmoja wa Rais
Donald Trump wa Marekani kutambua mji wa Jerusalem kuwa mji mkuu wa Palestina
ni "batili" na wameulaani kwa "kauli kali".
Rais wa Palestina Bw Mahmoud Abbas amesema kwa sasa Marekani sio
mpatanishi wa kweli wa amani.
Credit CRI Kiswahili





