POLISI WAMPOTEZEA MZEE WA 900 ITAPENDEZA 'DK SHIKA'
Kamanda
wa Polisi Kanda Maalumu yaDar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema kesi ya Dk
Louis Shika hawataendelea nayo kwa kuwa nyumba tatu za mfanyabiashara maarufu
Said Lugumi alizoahidi kuzinunua zote zipo.
Novemba 9, 2017 kampuni ya udalali ya Yono kwa niaba ya Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA) iliendesha mnada wa nyumba mbili za Lugumi zilizoko
Mbweni JKT na moja Upanga jijini Dar es Salaam ambazo zote Dk Shika alifikia
bei ya kuzinunua kwa Sh3.2 bilioni.
Mambosasa akizungumza leo Jumatano, amesema kesi yake haina
mashiko hivyo hawataendelea nayo kwa kuwa nyumba hizo zipo na hajatia hasara .
Amesema Dk Shika alikuwa akitamba kuwa ana fedha kumbe uwezo
wake ni mdogo na kusababisha kushindwa kulipa asilimia 25 kwa kila nyumba
hizo.
‘‘Dk Shika ni wa kumuonea huruma hana kitu tulisema
tunamchunguza na tutampeleka mahakamani lakini tumeona kesi yake haina mashiko
ndiyo maana hatuendelei nayo,” amesema Mambosasa.
Jeshi la polisi kanda hiyo lilimshikilia na kumwachia kwa
dhamana Dk Shika ambaye alikuwa akituhumiwa kwa kuharibu mnada baada ya
kushindwa kulipa asilimia 25 ya fedha hizo ambapo nyumba za Mbweni JKT alifika
bei kwa Sh900 milioni na nyingine Sh1.1 bilioni, huku ya Upanga alifika bei ya
Sh1.2 bilioni.
Chanzo- Mwananchi



