Breaking News

RIPOTI: UELEWA MDOGO JUU YA AFYA YA UZAZI NA UMASKINI, CHANZO CHA KUONGEZEKA KWA IDADI YA WATU DUNIANI

Naibu Waziri Wa Afya Maendeleo Ya Jamii, Jinsia, Wazee Na Watoto Dkt Faustine Ndungulile akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa ripoti ya hali ya watu duniani iliyondaliwa na shirika la umoja wa mataifa linaloshughulika idadi ya watu duniani UNFPA jijini dar es salaam.

Imeelezwa kuwa kasi ya ongezeko la watu nchini inatokana na jamii kutokuwa na elimu ya kutosha juu ya afya ya uzazi Hususani kwa wanamke waishio vijijini ni moja ya chanzo cha wanawake aliofikia umri wa kuzaa anazaa watoto zaidi ya wane.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Wa Afya Maendeleo Ya Jamii, Jinsia, Wazee Na Watoto Dkt Faustine Ndungulile wakati wa uzinduzi wa ripoti ya hali ya watu duniani iliyondaliwa na shirika la umoja wa mataifa linaloshughulika idadi ya watu duniani UNFPA jijini dar es salaam.

Alisema takwimu za utafiti wa hali ya afya ya watu ya mwaka 2015/16 inaonyesha kuwa kasi ya ongezeko la idadi ya watu ni asilimia 2.7, wakati hali ya uzazi ni wastani wa watoto watano kwa kila mwanamke aliye kwenye umri wa kuzaa.

“Wastani wa idadi ya wawatoto kwa wanawake asiye na elimu ni watoto saba wakati kwa upande wa wanawake aliyefika elimu ya sekondari ni watoto wanne, wale walio katika hali ya umaskini mama anazaa watoto nane ikilinganishwa na watoto watatu wa mama mwenye uchumi mzuri” alisema Ndungulile.
Mwakilishi Mkazi Wa UNFPA Nchini Bi Jacqueline Mahon akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa ripoti ya idadi ya watu duniani iliyondaliwa na shirika la umoja wa mataifa linaloshughulika idadi ya watu duniani UNFPA jijini dar es salaam.

Kwa upande wake mwakilishi mkazi wa UNFPA nchini Bi Jacqueline mahon alisema kumekuwepo na changamoto kubwa ya ongezeko kubwa la idadi ya watu duniani kutokana na kutokupo na usawa katika swala la kipato, rasilimali na haki.

“katika nchi nyingi ikiwemo Tanzania wanawake na wasichana wanakosa nafasi ya kufanya maamuzi juu ya masuala ya afya ya uzazi, maamuzi ya muda na wakati wa kushika ujauzito, ukizingatiwa usawa na ustwai wa watu wote ni msingi wa malengo endelevu ya dunia ili kuyafikia, tunahitaji kuwajengea uwezo wale amabo wanaonekana wapo nyuma hasa wananwake na wasichana“ Bi Jacqueline mahon.