CUF Wataka Wazee, Vingozi Wa Dini Na Viongozi Wataafu Wakutane Na Magufuli
Mwenyekiti wa Kamati ya
Uongozi CUF Taifa Bw. Julius Mtatiro akiongea katika mkutano wake na waandishi
wa habari (hawapo pichani) mapema leo 26 Feb 2017 jijini Dar es Salaam.
Dar es Salaam:
CHAMA cha Wananchi CUF
kimewataka Wazee, Viongozi Wa Stahafu Na Viongozi Wa Dini Akiwamo Kadinali
Polycarp Pengo wamshauri na kumpa nasaha Rais MAGUFULI arudi kwenye mstari
ili kulinusuru taifa na mwelekeo mbaya unaolikabili.
Mwelekeo
huo mbaya umetajwa kuwa ni kushamiri kwa mauji, utekaji na mashabulizi,
mashambulizi dhidi ya demokrasia, mihimili ya dola kuwekwa mfukoni mwa serikali,
hali ya uchumi wa nchi na kuvunjwa kwa haki na kukithiri kwa vitendo vya
upendeleo.
Kauli
hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa
CUF Julius Mtatiro alipokuwa akitoa taarifa zinazoeleza kuwepo kwa mwelekeo
mbaya wa taifa na kuishauri serikali.
“Taifa
letu linao wazee, linao waasisi, linao viongozi wastaafu. Kwa sababu mambo
hayako sawa kwenye nchi yetu, wazee wetu Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Warioba,
Butiku na wengine wote simameni na mwambieni JPM arudi kwenye mstari,”
“Hakuna
mtanzania ambaye angelipenda kupoteza muda wake kumkosoa rais na serikali yake,
lakini watanzania wanawajibika kufanya hivyo kwa sababu ya maamuzi ya rais na
utendaji wa serikali yake vinaathari za moja kwa moja kawa maisha ya kizazi
chetu na kijacho,” amesema na kuongeza Mtatiro.
Mauaji, Utekeji Na Mashambulizi
Mtatiro
amesema kuwa vitendo hivyo kwa sasa nchini ni mambo ya kawaida. Ameeleza kwamba
matukio hayo leo yakutisha ya mauaji yamelitia madoa ya damu serikali
lakini hadi sasa vyombo vyenye dhamana havina majibu ya matukio hayo.
Mashambulizi Dhidi Ya Demokrasia
Amesema
tangu kuingia madarakani kwa uongozi wa serikali ya awamu ya tano, kumekuwa na
jitihada kubwa za kuua demokrasia na mfumo wa vyama vingi hapa nchini na amedai
kuwa juhudi hizo zinafanywa na rais Magufuli.
Mihimili Ya Dola Kuwekwa Mfukoni Mwa Serikali
Mwenyekiti
huyo wakamati ya uongozi amedai kuwa mhimili mmoja (serikali) umejipa mamlaka
makubwa kiasi cha kudhibiti mihimili mingine. Ametoa mfano kwa kusema serikali
kwa sasa inapanga mipango mingi na inatumia fedha nyingi za taifa bila
kulihusisha bunge. Hivyo imelidhibiti bunge na mahakama pia imedhibitiwa.
Hali Ya Uchumi Wa Nchi
Amedai,
hali ya uchumi kwa sasa inaanguka kutokana na kwamba mzunguko wa fedha ni
mdogo, hali mbaya ya biashara, mfumuko wa bei za bidhaa za vyakula na mabenki
kufungwa, hivyo amesema kama hatua isipochukuliwa taifa litaenda kubaya.
Kuvunjwa Kwa Haki Na Kukithiri Kwa Vitendo Vya
Upendeleo.
Amesema
utawala wa awamu hii chini ya rais Magufuli unaongoza taifa kwa kuwa na “double
standard”, kujuana na upendeleo ambapo alitoa mfano wa bamoa bomoa iliyowafanya
kwa wakazi wa kimara jijini Dar es Salaam kwa madai ya kuvamia hifadhi ya
barabara huku juzi rais akisitisha bomoa bomoa kwa wakazi wa Mwanza waliovamia
eneo la uwanja wa ndege.



