TTCL Corporation Yaja Na Huduma Mpya Ya (Fiber Connect Bundle) Yenye Kasi Ya Ajabu
Mkurugenzi
MKuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation) Bw. Waziri Waziri
Kindamba akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani), kulia ni Bw.Ali
Mbega Mkuu wa Mauzo na Masoko (TTCL Corporation) makao makuu ya shirika hilo jijini
Dar es salaam.
Dar es salaam.
Shirika La
Mawasiliano Tanzania (TTCL), Leo limezindua huduma mpya ya intanet
yenye kasi zaidi iliyopewa jina la Fiber Connect Bundle ikiwa ni moja ya mwendelezo
wa utoaji huduma kipekee, zenye bora na za kibunifu za Kampuni hiyo ya
kizalendo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo Jijini dar es salaam Mkurugenzi
wa Shirika hilo Bw. Waziri Kindamba alisema Kupitia kifurushi cha Fiber
Connect, Mteja ataweza kufaidika na huduma zifuatazo; Kwanza, Mteja atapata
Intaneti yenye kasi isiyo na kikomo (Unlimited).
“Kupitia huduma hii
mpya ya Fiber Connect Bundle, ambayo itakuwa ya kasi zaidi mteja wetu atapata
huduma nne kwa pamoja zikiwa na unafuu mkubwa wa gharama na ubora wa hali ya
juu” Alisema Bw. Kindamba.
Alisema tayali
shirika hilo limeanza kuchukua hatua kuwafikia wateja wa majumbani na kufanya
mapinduzi makubwa ya kimawasiliano ambapo kwa kuanzia, mradi unatarajiwa
kufikisha huduma katika nyumba zipatazo 500 katika eneo la Mikocheni, na
nyumba 500 zingine katika eneo la Mbezi Beach na nyumba zaidi ya 200 katika
eneo la Medeli Mkoani DODOMA.
Akizungumzia mwelekeo wa utendaji wa Shirika Bw. Kindamba alisema
unaonesha ukuaji mzuri licha ya changamoto zilizopo Mapato yameendelea
kuongezeka na hasara kupungua kwa kiasi kikubwa, jambo linalotupa uhakika wa
kutimiza ahadi yetu ya kutoa gawio Serikalini katika mwaka huu wa fedha
2017/2018.
“Mtakumbuka kuwa, kwa zaidi ya miaka kumi na tano iliyopita, TTCL
haikuawahi kutoa gawio, Tumedhamiria kuvunja mwiko huu kwa kutimiza ahadi yetu
kwa Umma ya kutoa gawio la shilingi Bilioni moja katika mwaka huu wa fedha” Alisema
Kindamba.
Mkuu
wa Mauzo na Masoko (TTCL Corporation) Bw. Ali Mbega akitoa ufafanuzi kwa
waandishi wa habari (hawapo pichani) Kulia kwake ni Mkurugenzi MKuu wa Shirika
la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation) Bw. Waziri Waziri Kindamba.
Bw Kindamba aliongeza
kuwa Menejimenti ya shirika hilo itaendelea kuweka mkazo katika kuboresha eneo
la Huduma kwa Wateja kwa kutoa huduma bora kwa gharama nafuu, kuongeza Wateja
wapya, kusambaza huduma za 4G LTE katika Makao Makuu ya Mikoa yote Nchini
ifikapo Juni 2018.
Aidha, tutaendelea kuongeza uwekezaji katika Teknolojia na Miundo mbinu
yetu kote nchini, kuboresha mazingira ya kazi kwa Wafanyakazi na Vitendea kazi,
kukusanya Madeni ya Shirika, kuongeza Wateja na ufanisi katika huduma za fedha
Mtandao (TTCL PESA) na kuongeza ufanisi katika Miundombinu ya Kimkakati ya
Serikali inayosimamiwa na kuendeshwa na Shirika la Mawasiliano Tanzania na hapa
ninazungumzia Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano (NICTBB) na Kituo Mahiri cha
kuhifadhia Kumbukumbu(National Data Centre).
Aliongeza kuwa Kupitia huduma hiyo mpya Mteja atapata huduma ya simu za
sauti kwa simu za mezani na (Sim card) ambayo ataitumia kwenye simu yake ya
mkononi na kupata huduma ya Intaneti sawa na simu ile anayopata katika simu ya
mezani.
Pia Mteja atapata
huduma za wireless service (WiFi) katika nyumba yake ambapo vifaa vyote
vinavyotumia Teknolojia ya Intaneti vitaunganishwa na kuweza kutumia huduma
hii. Mfano wa vifaa husika ni Smart Tv, Tablets, Laptops na kadhalika, sambamba
Mteja atapatiwa vifaa vyote bure pamoja na uhakika wa huduma za baada
(After Sells Services) endapo itahitajika.
Jina la Kifurushi
|
Muunganiko wa Huduma
|
Gharama
|
Matumizi
|
|
Kasi ya Intaneti (Mbps)
|
Dakika za maongezi Mitandao yote
|
|||
Fiber Connect Lite
|
10
|
50
|
100,000.00
|
Siku 30
|
Fiber Connect Basic
|
30
|
100
|
150,000.00
|
|
Fiber Connect Preffered
|
50
|
300
|
200,000.00
|
|
Ili kupata
huduma ya kifurushi hiki maalumu cha FTTH, Mteja unapaswa kufanya yafuatayo;
Piga namba 100/ 022214100100 kuongea na Wahudumu wetu au
Tembelea
kituo chetu cha Huduma kwa Wateja kilicho karibu nawe.
Huduma hii
inazilenga: Taasisi zote za Serikali, Wafanyabiashara wakubwa, wa kati na
wadogo na Ofisi mbalimbali.





