Mhe Zitto Amepost Ujumbe Huu.. Mara Baada Ya Kutajwa Katika list Ya Watu Wenye Nia Mbaya Kwa Taifa.
Ujumbe
wa Mhe Zito Kabwe aliopost leo katika mtandao wa twiter mara baada ya kushutumiwa na Bw. Cyprian Majura Musiba
Hii Hapa kauli ya Musiba….
Mkurugenzi wa Kampuni ya CZI, Cyprian
Majura Musiba amesema kuwa Mange Kimambi anatumiwa na FBI hivyo vyombo vya dola
havitakiwi kumpuuzia bali vinatakiwa kumshughulikia kabla ya madhara hayajatoke
kwa sababu amekuwa akiratibu shughuli mbalimbali za kutaka kuipindua serikali.
Ameyasema hayo mapema hii leo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na
waandishi wa habari ambapo amesema kuwa amani ni kitu cha msingi katika taifa
Amesema kuwa watu wenye nia mbaya ya kutaka
kuharibu amani ya nchi kwa maslahi yao binafsi na kwa kutumiwa na watu wa
mataifa ya nje hawatakiwi kuvumiliwa hata kidogo kwani nchi ikipata machafuko,
wao watakimbilia nje ya nchi na kuwaacha wananchi masikini wakitaabika.
“Mange Kimambi kwa taarifa zilizopo anatumiwa
na shirika la Kijasusi la Marekani FBI, Mange Kimambi ni wa kushughulikiwa,
nchi ikipata machafuko yeye anaendelea na shughuli zake za aibu anazozifanya
huko, kwani nani hajui kwamba Mange anafanya shughuli hizo kwa Marekani na
analipia kodi, kwa Marekani biashara hiyo inatambulika,”amesema Musiba.
Mtizame katika Video hii ====>>
Mtizame katika Video hii ====>>




