TGNP Mtandao Kufanya Kongamano Kubwa La Wanawake Na Uongozi February 27 Jijini Dar.
Mkurugenzi Mtendaji Wa Mtandao Wa Jinsia (TGNP) Bi. Lilian Liundi .
Dar es salaam.
TGNP Matandao kwa
kushrikiana na wadau wengne wa maswala ya kijinsia wameandaa kwa mara ya kwanza
kongamano la wanawake na uongozi ambalo litafanyika 27 mwezi huu katika ukumbi katika
ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam.
Akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam Mkurugenzi Mtendaji
Wa Mtandao Wa Jinsia (TGNP) Bi. Lilian Liundi alisema kongamano hilo la siku
moja ambalo linafanyika kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa shirika hilo
miaka 25 iliyopita litakutanisha wanawake zaidi ya 250 walio katika nafasi mbalimbali
za uongozi na waliostafu.
“Lengo
kuu la Kongamano hili ni kuwakutanisha wanawake kwa pamoja kuweza kujadili
namna gani wataweza kuongeza nafasi za uongozi na maamuzi kwani bado hawajaweza
kufikia lengo ambalo ni 50 kwa 50, sambamba na kutambua, kusherekea na
kuimarisha ushiriki na hamasa hamasa ya wanawake katika vyombo vya katika ngazi
za kijamii na kitaifa” alisema Bi Liundi.
Alisema
pia washriki watajadili changamoto mbalimbali anazokutana nazo mwanamke katika
Nyanja ya elimu, afya na umiliki wa ardhi swala ambalo bado ni changamoto kubwa
kwa wanawake wengi hivi sasa, pamoja na kuenzi na kukumbuka mchango uliotolewa
na wanawake ambao walikuwa katika ngazi za uongozi maamuzi kuanzia ngazi ya
jamii mpaka taifa.
Mkurugenzi Mtendaji wa
TGNP Mtandao Bi. Lilian Liundi (katikati) akiwa na jopo la wafanyakazi wa
shirika hilo pamoja na wadau mbalimbali walioshiriki katika kuandaa Kongamano
la Wanawake na Uongozi.
Aidha
Bi.Liundi aliongeza kuwa kongamano hilo pia litatoa fursa ya kipekee kutafakari
kuhusu kazi zisizo kuwa na kipato kama kulea familia wazazi, wagonjwa na watu
wanaoishi na ulemavu kwani uchunguzi umebaini kuwa wanawake hutumia muda wa
masaa 10 mpaka 15 kwa siku kwa shughuli hizo hivyo kukosa muda wa kufanya
shughuli za kujipatia kipato.
Mgeni
Rasmi katika Kongamano hilo anatarajiwa kuwa Waziri msataafu Mhe. Marry Nagu, sambamba
na viongozi wa sasa na wastaafu,wabunge, madiwani, watia nia wa uongozihasa
vijana wa kike katika kuhakikisha
kongamano hilo linaleta tija kwa jamii yetu.



