TECNO KUZINDUA TOLEO JIPYA?
Paparazi tayari wameshaanzisha uvumi kama ilivyo ada,
ambapo safari hii wakiihusisha kampuni kinara katika uzalishaji wa simu za
mkononi TECNO,ikitajwa zaidi midomoni mwa watu, tetesi zaidi zinaihusisha
kampuni hiyo pendwa na ujio wa toleo jipya ikiwa ni muendelezo wa jamii ya
Camon inayosemekana kuzinduliwa nchini Nigeria, siku na saa bado havikuwekwa
wazi.
Inasemekana kwamba simu hiyo itaendana na uchumi wa Afrika
ikikadiriwa kuwa na bei nafuu, hivyo nadhani wa Afrika wanacho cha kujivunia.

Swali ni kwamba je ni kweli TECNO watakuja na toleo jipya
kama inavyosemekana midomoni mwa wadau mbali mbali, bado hakujakuwa na taarifa
rasmi kutoka kwenye vyanzo vya kuaminika

Mara nyingi TECNO inapohusishwa kuhusu toleo jipya bhaasi
huwa kweli,je awamu hii TECNO wanakipi cha tofauti? Maswali yamekua mengi
yakiacha wadau vinywa wazi wakiwa na shauku ya kutaka kuona ni nini TECNO
watakachoingiza sokoni ikiwa ni muendelezo wa Camon.
Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti ya http//www.tecno-mobile.com/tz



