Tetesi Za Soka Ulaya Leo Alhamisi..
Gareth Bale
Na Mashirika
ya kimataifa
Winga wa Real Madrid Gareth Bale, mwenye umri wa miaka 28, ameshawishiwa na meneja wa Manchester United Jose Mourinho kujiunga na klabu hicho ya Ligi ya Premia mwisho wa msimu. (Marca). Wakati huo huo, Bale ameambiwa na kocha wa Wales Ryan Giggs aendeshe kiti maalum ili kujiepusha na majeraha. (Times)
Winga wa Real Madrid Gareth Bale, mwenye umri wa miaka 28, ameshawishiwa na meneja wa Manchester United Jose Mourinho kujiunga na klabu hicho ya Ligi ya Premia mwisho wa msimu. (Marca). Wakati huo huo, Bale ameambiwa na kocha wa Wales Ryan Giggs aendeshe kiti maalum ili kujiepusha na majeraha. (Times)
Manchester City
wanatarajia kuanzisha mazungumzo kuhusu mkataba mpya na winga Raheem Sterling,
mwenye umri wa miaka 23, kabla ya kumalizika kwa msimu . Mchezaji huyo wa
kikataifa wa England ana miaka miwili iliyosalia kwenye mkataba wake. (ESPN)
Tottenham
wanamtaka mchezaji wa kiungo wa kati wa Lisbon Bruno Fernandes, mwenye umri wa
miaka 23, lakini watatakiwa kulipa kitita cha Euro milioni 87 kusaini mkataba
na mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno . (Abola - kwa Kireno)
Arsenal imefanya
mazungumzo juu ya kuhamia kwa mlinzi wa Freiburg Caglar Soyuncu, mwenye umri wa
miaka 21. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uturuki amethamanishwa kwa kiwango cha
Euro milioni 30 na kilabu cha Bundesliga . (Mail)
Chelsea
wanakaribia kusaini mkataba na kijana wa Uholanzi Jayden Braaf, mwenye umri wa
miaka 15, kutoka timu ya PSV Eindhoven. Manchester City, Manchester United,
West Ham na Bayern Munich wote wameelezea nia yao ya kuwania saini ya
mshambuliaji huyo. (Mail).
Everton wanaongoza
katika kinyang'anyiro cha kusaini mkataba na mchezaji wa kiungo wa kati wa
Arsenal Jack Wilshere, mwenye umri wa miaka 26, ikiwa ataondoka kwenye kilabu
hicho katika msimu huu wa majira ya joto . Mkataba wa mchezaji huyo wa
kimataifa wa England unakwisha msimu huu wa majira ya joto. (Star).
Everton wana mzozo
wa mkataba na meneja wa zamani wa timu hiyo Ronald Koeman, ambaye kwa sasa ni
meneja wa timu ya Uholanzi Netherlands, baada ya kubainika kuwa kilabu hicho
kinalipa 90% ya malipo aliyolipwa Muholanzi huyo. (Liverpool Echo).
Watford huenda wakamuuza
kwa kiwango cha Euro milioni 40 mchezaji wa kiungo wa kati Abdoulaye Doucoure,
mwenye umri wa miaka 25, katika msimu huu wa majira ya joto, huku Liverpool,
Tottenham na Arsenal wote wanammezea mate mFaransa huyo. (Mirror).
Mchezaji wa kiungo
cha kati wa Stoke Ibrahim Afellay, mwenye umri wa miaka 31, ameambiwa awe mbali
na klabu hiyo na Paul Lambert, ambaye hapendezwi na tabia ya Mholanzi huyo na
kiwango chake katika mazoezi. (Telegraph)
Striker Zlatan
Ibrahimovic, mwenye umri wa miaka 36, aliondoka Manchester United baada ya
kushindwa kuendelea katika ligi ya klabu bingwa Ulaya, kulingana na daktari
aliyemfanyia upasuaji ya goti la mchezaji huyo wa Sweden. Amejiunga na LA
Galaxy. (South China Morning Post).
Manchester United
wanaangalia uwezekano wa kusaini mkataba na mchezaji wa kiungo cha kati wa
Tottenham Chukwunonso Madueke, mwenye umri wa miaka 16, baada ya kukataa
kusaini mkataba mpya na kilabu hicho cha kaskazini mwa London. (Mail).
Meneja wa Italia
Carlo Ancelotti amekataa kuchukua kazi ya kuiongoza timu ya taifa hilo kwani
anasubiri kurejea katika Ligi ya Premia ya Ulaya, huku chaguo lake likiwa ni
klabu za Chelsea na Arsenal (ItaSportPress - kwa Kitaliano).
Mchezaji wa kiungo
cha kati wa Juventus Claudio Marchisio, mwenye umri wa miaka 32, anaweza
kuondoka katika kilabu hicho kujiunga na MLS ya New York City. Mkataba wa
mchezaji huyo wa kimataifa wa Italia katika Turin unamalizika msimu huu wa
majira ya baridi. (Tutto Mercato Web - in Italian).
Mkurugenzi wa soka
wa timu ya Aston Villa Steve Round anasema nahodha John Terry ameashiria kuwa
ataendelea kuwa na kilabu hicho. Mlizi huyo wa zamani wa England, mwenye umri
wa miaka 37, amekuwa akitarajiwa kustaafu na kurejea katika kilabu cha Chelsea
kama kocha. (Birmingham Mail).



