Breaking News

Wazir Mwakyembe Ametoa Maamuzi Haya Sakata La Kufungiwa Kwa Roma.


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt harrison mwakyembe leo Machi 29, 2018 ametangaza kumsamehe msanii wa muziki Roma Mkatoliki adhabu yake ya kufungiwa muziki.

Msanii huyo alifungiwa kujihusisha na shughuli za muziki kwa muda wa miezi 6 kwa kosa la kutotii amri aliyokuwa amepewa na BASATA la kurekebisha baadhi ya maneno katika wimbo wa "Kibamia".

Mwakyembe amesema kuwa adhabu ya Roma itaisha muda wowote atakapokabidhiwa hati ya usajili ya Baraza la Sanaa nchini (BASATA).