MKE WA NANE WA MFALME MSWATI AJIUA

Mke wa
nane wa Mfalme Mswati wa Swaziland Senteni Masango, amejiua Ijumaa ya wiki
iliyopita, wa kunywa dawa za vidonge aina ya amytriptyline, ambazo ndizo
zilizoondoa uhai wake.
Malkia
huyo amejiua wiki moja baada ya kuhudhuria mazishi ya dada yake Nombuso
Masango, ambapo tetesi zinasema kwamba Mfalme alimkataza kuhudhuria mazishi
hayo.
Habari
zaidi zinasema kwamba mke huyo ambaye aliolewa mwaka 1999 na kuwa mke wa 8 wa
Mfalme Mswati, alikuwa akiishi kwenye kasri ya Kifalme peke yake kwa takriban
miaka mitatu, bila kutembelewa na mume wake huyo.
Tayari
Malkia huyo wa Swaziland ambaye alikuwa miongoni mwa wake vipenzi wa Mfalme
Mswati amezikwa kwenye eneo la kifalme la Swaziland, huku Mfalme Mswati
akiendelea kupokea salamu za pole kwa viongozi mbali mbali wa serikai.
Habari
zinasema kwamba Mfalme Mswati alishawahi kukimbiwa na wake wawili kwa tuhuma za
unyanyasaji, huku wengine akiwapa adhabu kali ikiwemo kutengwa na kasri ya
Kifalme.



