Musiba Awashukia TEF, Awataka Kutotumika Kisiasa

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya CZI
Limited, Cyprian Musiba amelitaka Jukwaa la Wahariri kujitathmini na
kujitafakari kuhusiana na matamko mbalimbali wanayoyatoa.
Ameyasema hayo wakati akizungumza na
waandishi wa habari mjini Dodom, ambapo amesema kuwa ni vyema Jukwaa hilo la
Wahariri likajikita katika kuwasaidia waandishi wa habari.
Amesema kuwa Jukwaa hilo lina wajibu
mkubwa wa kuwasaidia waandishi wa habari kuboresha maslahi yao lakini si
kutumika kisiasa na kuichafua serikali.
Aidha, Musiba ameongeza kuwa TEF
imekuwa ikitoa matamko mbalimbali ambayo hayana uhusiano wowote na waandishi wa
habari, hivyo ameliasa kujikita zaidi katika kuangalia namna na kutetea maslahi
ya waandishi kuliko kutumika kisiasa.
“Press Club hawajui, UTPC hawajui
halafu wewe unatoa tamko, uandishi wa habari sio Dar es salaam peke yake, ni
Tanzania nzima, ninachowashauri TEF tuwatengenezee waandishi wa habari
mazingira mazuri ya kazi,”amesema Musiba
Hata hivyo, Musiba ameongeza kuwa
Jukwaa la Wahariri (TEF) hawatakiwi kulalamika kuhusu kukosa wadhamini bali
wanatakiwa kujikita katika kujenga misingi imara ya waandishi wa habari na si
kutumika kisiasa kama wanavyofanya kwasasa.



