MAHAKAMA Yamwachia Huru Aliyeiba Mahindi Yakanasa Kichwani

Mahakama ya Mwanzo Mlandizi mkoani Pwani imemuachia
huru, kijana Frank Joseph (23) aliyeiba kiroba cha Mahindi debe 1 na kumnasia
kichwani baada ya mlalamikaji kutofika mahakamani hapo mara 3 mfululizo.
Frank ambaye ni mkazi wa Mbezi Dar es salaam,
ameachiwa huru na Hakimu Mfawidhi, Nabwike Mbaba wakati shauri hilo
lilipoitishwa kwa ajili mlalamikaji (mtendewa) kutoa maelezo ya jinsi
alivyoibiwa.
Hakimu Mbaba amesema kuwa kutokana na mlalamikaji
(mtendewa) kushindwa kufika mahakamani hapo mara 3 mfululizo kutoa maelezo ya
kuibiwa kwake anaifuta kesi huyo.
“Mtendewa ameshindwa kufika mahakamani licha ya
kupewa wito mara 3 mfululizo, hivyo naifutilia mbali kesi hii na mshtakiwa kuanzia
sasa upo huru,” amesema Hakimu Mbaba.
Awali mshtakiwa alishindwa kufikishwa mahakamani
mara 2 mfululizo kutokana na gari la Magereza kuharibika.
Katika kesi hiyo namba 124/2018 Frank anadaiwa
kutenda kosa la wizi May 3, 2018 saa 7 usiku maeneo ya Mlandizi ambapo aliiba
Mahindi debe 1 likiwa na thamani ya Sh.20, 000 ikiwa mali ya Seve Seleman.



