Yanga Kumalizana Na Nyota Huyu Wa Simba…

BAADA ya siku chache kudaiwa kuwa, kiungo wa Simba, Mohamed Ibrahim ‘Mo’
amesajiliwa Yanga imebainika kuwa dili hilo linatarajiwa kukamilishwa rasmi leo
Jumatano, baada ya pande mbili kukutana na kuweza kumalizana.
Mo tayari ni mchezaji huru kwa sasa kutokana na
mkataba wake kumalizika mwezi ujao na amekuwa hana nafasi ndani ya kikosi cha
Simba.
Akizungumza nasi meneja wa mchezaji huyo,
Jamal Kisongo alisema anatarajia kukutana na viongozi wa klabu hizo ili kuweza
kujadiliana.
“Suala la Mo litafahamika rasmi sababu
mchezaji alikuwa kwenye mechi kule Songea na ndiyo anarejea
hapa Dar kwa mapumziko, hivyo kila kitu kuhusu yeye kitajulikana tu baada ya
kukutana pande mbili sababu alipata ofa kadhaa.
“Sababu mkataba wake na Simba ndiyo huo unamalizika
na ligi imekwisha, hivyo tutajua mustakabali wake kwa ujumla msimu ujao utakuwa
ni kwa klabu ipi na tunachohitaji ni mchezaji kupata timu na kuweza kuendeleza
kipaji chake,” alisema.
Source : Champion,



