Breaking News

List Ya Kikosi Cha Simba Kilichokwenda Kenya Hiki Hapa


Kikosi cha Simba kimeondoka leo kuelekea Kenya kwa ajili ya kushiriki michuano ya Sportpesa Super Cup, inayotarajiwa kuanza June 03 hadi June 10 ikizihusisha timu nane huku 4 zikitoka Tanzania na 4 za Kenya.
Timu zote zinazoshiriki michuano hii ni zile zinazodhaminiwa na kampuni ya Sportpesa ambapo kwa Tanzania ni Simba, Yanga, Singida United na JKU ya Zanzibar.
Katika michuao hiyo inayoanza June 03 katika hatua ya mtoano, Bingwa atajinyakulia kitita cha Milioni 68 pamoja na kupata nafasi ya kusafiri kwenda nchini Uingereza kucheza na Everton inayoshiriki ligi kuu nchini humo ya EPL, huku mchezo huo ukitarajiwa kufanyika kwenye dimba la Goodison Park.
Hiki Hapa Kikosi Kamili Kilichoondoka:
Aishi Salum Manula, Said Mohamed Nduda’,Ally Salim, Ally Shomary, Shomary Salum Kapombe, Mohamed Hussein Jr, Paul Bukaba, Erasto Edward Nyoni naYusuph Mlipili.
Wengine ni Said Hamis Ndemla, Jonas Gerald Mkude, Mzamiru Yassin, Rashid Juma, Haruna Niyonzima, Mohamed Ibrahim ‘Mo’, Moses Kitandu na Marcel Kaheza Bonaventure na Shiza Ramadhan Kichuya.
Katika kikosi hicho ukimtoa Niyonzima tu, nyota wengine wote wa kigeni hawakuweza kusafiri pamoja nahodha wa kikosi hicho John Bocco, huku taarifa zikidai kuwa wachezaji hao wana ruhusa maalum
Pia imefahamika kuwa nyota mpya kutoka Lipuli Fc Adam Salamba na Nahonda wa kikosi hicho John Raphael Bocco wataungana na kikosi hicho Jumapili  kabla ya mashindano hayo kuanza Jumapili ya June 03 mwaka huu