Manispaa ya Ubungo Na TBA Wasaini Maktana Wa Bili 6.2 kujenga ofisi za Manispaa.
Mkuregenzi wa Manispaa ya Ubungo Bi.Beatrice Kwai na Meneja wa Wakala wa Majengo Nchini (TBA) Mkoa wa Dar es Salaam, bw. Edwin Godfrey wakibadilishana hati za makubaliano ya ujenzi ofisi ya manispaa hiyo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Meya wa Manispaa ya Ubungo Boniface Jacob.
TBA na Manispaa ya Ubungo wakisaini Mkataba ya makubaliano ya ujenzi wa Manispaa hiyo jijini Dar es Salaam
Meya wa Manispaa ya Ubungo Boniface Jacob akifafanua jambo kwa waandishi habari mara baada kutiliana saini ya makubaliano ya ujenzi wa Manispaa hiyo jijini Dar es Salaam
Mkuregenzi wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Kwai akitoa maeleza juu ya mradi huo utakavyotekelezwa mara baada ya kutiliana saini jijini Dar es salaam.
Dar es salaam:
Halmashauri ya Manispaa ya ubungo imeingia mkataba na wakala wa majengo nchini (TBA) wenye thamani ya tsh Bilioni 6.2 kwa ajili ya mradi wa Ujenzi wa jengo la ofisi litakalotumiwa na Halmashauri hiyo.
Akizungumza mara baada ya kusaini makubaliano hayo jijini Dar es salaam meya wa ubungo mhe Boniface Jacob alisema anatumaini ujenzi huo utakamilika kwa wakati kama mkataba unavyo onyesha hivyo kumaliza changamoto ya mda mrefu ya kupangisha.
Alisema mradi huo utekelezwaji wake Serikali Kuu itatoa Bilioni 4.3 na Halmashauri kupitia mapato yake ya ndani Sh.bilioni 1.9 hivyo kuwataka wakala wa majengo kukamilisha ujenzi huo kwa wakati kutokana na Halmashauri hiyo imekuwa ikilazimika kwa sasa kukodi jengo la halmashauri hiyo kwa kiasi cha Milioni 192 kila mwaka.
"Nitoe tahadhali kwa TBA mkajipime kabla hamjaanza ujenzi kwani mkionyesha kusuasua mimi ndio ntakuwa wa kwanza kulalama kwa vile wadau wetu wa pili wa mradi huu ambao ni Serikali wamewateua nyie mjitahidi msiwaangishe ili kuendelea kuwa na imani na nyie". Alisema Meya Jacob.
Mhe Jacob aliongeza kuwa awali wananchi walikuwa wakitembea kilometa 30 kwenda kupata huduma lakini ujenzi huo utakapokamilika kusogeza huduma sambamba na kuinua uchumi wananchi kwa kutoa kitoa ajira kwa wakazi kipindi cha ujenzi wa mradi huo.
Kwa upande wake, Meneja wa wakala wa majengo TBA Mkoa wa Dar es Salaam, bw. Edwin Godfrey alisema atahakikisha wanafanyakazi kwa weledi iwe jua, mvua au sikukuu watakuwa eneo la kazi ili kukamilisha mradi huo kwa wakati na kiwango kinachotakiwa.
"Tumepokea maagizo yote tunachoahidi ni iwe nvua, jua, usiku, sikukuu tutafanyakazi masaa yote kwa kiwango kinachohitajika ambacho kipo kwenye mikataba yetu". alisema Godfrey.
Mapema akizungumza mara baada ya utiaji saini mkataba huo mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Bi. Beatrice Kwai alisema akiwa kama mtendaji mkuu wa manspaa hiyo atahakikisha anasimamia utekelezaji wa mkataba kwa viwango vinavyotakiwa.
"Halmashauri wamejipanga kutoa malipo ya gharama zote za mradi huo ili utekelezwe kwa wakati ninachoomba mkandarasi ahakikishe anatimiza wajibu wake katika kipindi chote cha ujenzi wa mradi huo,"alisema Beatrice.



